Mbwana Samatta kapewa mkataba mpya KRC Genk

Club ya KRC Genk imetangaza good news kuhusiana na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye anaichezea club hiyo, KRC Genk imeonesha kuendelea kumuamini Mbwana Samatta na imeamua kumuongezea mkataba mpya staa huyo.

Samatta ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea KRC Genk, hivyo kutokana na mkataba wake wa awali kumalizika mwishoni mwa msimu 2018/2019, kutokana na kuongeza kwa mkataba huo atakuwa Luminus Arena hadi mwaka 2021.

No comments

Powered by Blogger.