TCU imevifuta vyuo vikuu viwili

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha masomo na udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo na katika programu kwenye baadhi ya vyuo vikuu nchini kutokana na kukosa vigezo. Na kuvifuta vituo viwili vya vyuo vikuu na kuamuru wanafunzi wanaoendelea na masomo wahamishiwe kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa TCU, Prof.Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM leo ambapo amevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu kishiriki cha Marian (MARUco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vingine ni Chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), Chuo kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania (SJUT-St. Marks Centers na Chuo kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT). Pamoja na Chuo kikuu Teofilo Kisanji, Kituo cha Tabora  na Chuo kikuu Mt. Yohana cha Tanzania, Msalato (SJUT -Msalato Center).

Mbali na hayo amevitaja vyuo vilivyositishiwa utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe kuwa ni Mlima Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo cha Eckernforde Tanga (ETU) cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta Kituo cha Arusha na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah kibira (JOKUCo).

Nae mwakilishi wa bodi ya mikopo (HELSB), Deus Changala amesema waliokuwa na mikopo wasiwe na wasiwasi itawafata vyuo watakavyohamishiwa.

No comments

Powered by Blogger.