“Msije kufikiri sipendi matajiri, waliopata utajiri wao kihalali” JPM
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
ameendelea na ziara yake katika mikoa ya Mwanza na Mara kwa kufungua
viwanda 3 vya kampuni ya Lakairo, kuzindua ujenzi wa kiwango cha lami
kwa barabara ya Bulamba – Kisorya (51km), kufungua mradi wa maji katika kijiji cha Nebuye kwa ajili ya wananchi wa Nansio.
Viwanda vya kampuni ya Lakairo vilivyopo katika eneo la Isangijo Wilaya ya Magu vinajumuisha kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya nafaka, kiwanda cha pipi na jojo na kiwanda cha ‘steelwire’ ambavyo ni uwekezaji wa Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo (Lakairo), uliogharimu Bilioni 20.1 na vimeajiri watu 400.

No comments