Ridhiwani Kikwete akanusha taarifa za wanaotaka kumgombanisha na Kiongozi wake mitandaoni

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekanusha kutoa ujumbe uliokuwa unasambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kupost video katika akaunti yake ya Instagram yenye caption isemayo. “Ikumbukwe Watanzania wenzangu na ususani WanaCCM wenzangu, mapema mwanzoni  mwa Mwaka huu 2018, tarehe 22 niliutaarifu umma ukweli juu ya kile nilichokiita maneno ya kiuchonganisha yanayolenga kunigombanisha Mimi na Uongozi wa Chama changu CCM.”

“Kupitia ujumbe mdogo wa Video nilikanusha juu ya maneno hayo kwamba  sikuyaandika mimi na wala sina uhusiano wowote na maneno hayo. Lakini la kushangaza baada ya miezi Saba, jambo hilo linaibuka tena leo.”-Ridhiwani

“Ndugu Watanzania wenzangu napenda kuwahakikishia kuwa sihusiki na Maneno hayo na Ninawaomba sana muyapuuze.” amehitimisha Ridhiwani

  

No comments

Powered by Blogger.