Rais Kikwete alivyoondoka TZ leo kuelekea Zimbabwe kumuwakilisha JPM Magufuli
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea Harare nchini Zimbabwe ambapo anakwenda Kumuwakilisha Rais Magufuli kwenye Sherehe za kuapishwa Rais Zimbabwe Emmerson Mnangagwa zinazofanyika leo tarehe 26 Agosti, 2018 katika uwanja wa michezo waTaifa Mjini Harare.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege Rais Mstaafu Kikwete ambaye amefuatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Philip Mangula na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo , amesema
Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu
kwani katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya
wananchi wake waliwahi kuishi nchini Tanzania, husasani wanachama wa
Chama cha ZANU PF, na kupata mafunzo hapa nchini.
No comments