Waziri Mkuu aikabidhi Wizara ya Kilimo Matrekta 500
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amemkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.
Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo
nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo
inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na
matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe
ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.
“Katika
kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima
walichelewa kuanza kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi
wanadhoofu sana,” -Dkt Tizeba
“Mara
mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate
nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia
teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho
kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” -Dkt. Tizeba
Tizeba
alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja
mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa
kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia
ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji
wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.
No comments