RC TEMEKE AWAMWAGIA SIFA WOISO ORIGINAL PRODUCTS KWA KUNYAKUA TUZO YA BIDHAA ZA NGUO NA NGOZI
MKUU
wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka wananchi hasa watokao
katika Manispaa ya Temeke kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonesho ya
42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba ili kujipatia elimu ya
ujasiriamali.
Lyaniva
ametembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo na kujionea kazi za
wazalendo wakiwa na bidhaa tofauti zilizotengenezwa hapa nchini
wakitilia mkazo kauli ya Rais wa John Pombe Magufuli ya uchumi wa
viwanda.
Akizungumza
na Globu ya Jamii akiwa ndani ya banda la bidhaa za nguo na ngozi la
Woiso Orginal Company Ltd Lyaniva ameeleza kuwa maonesho hayo
yameboreshwa na washiriki wamekuwa wengi kutoka katika nchini mbalimbali
duniani.
"Maonesho
ya mwaka huu zaidi ya mataifa 50 kutoka nje ya nchi wameweza kushiriki
na wameleta bidhaa bidhaa nzuri zikiwa zenye ubora wa hali ya
juu,"amesema Lyaniva.
Lyaniva
amewapongeza wazalishaji wa bidhaa za nguo na ngozi kutoka kampuni ya
Woiso Original Products kwa kuzalisha bidhaa nzuri na zenye ubora wa
hali ya juu na kwa bei nzuri ambayo unanunua kitu na utadumu nacho kwa
mda mrefu na amewataka wananchi kujitokeza sasa kuona na kujifunza namna
bidhaa za kitanzania hasa za ngozi zilivyoshika hatamu kwa ubora wa
hali ya juu.
Aidha
amewashukuru watanzania walioelewa na kuunga mkono juhudi za Rais
Magufuli katika masuala ya kiuchumi na wamekuja vizuri sana na kuboresha
maonesho hayo ambayo kwa namna moja au nyingine yana tija kwa taifa
letu.
Naye
Meneja masoko wa Woiso Original Products Company Ltd bi. Teya Herman
ameeleza kuwa wao kama kampuni wanajituma sana katika kuhakikisha
wanatoa bidhaa bora za ngozi na nguo kama vile viatu, mikanda, pamoja na
nguo na mapazia.
Kuhusu
tuzo waliyokabidhiwa leo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 42 ya
Kimataifa ya Biashara Sabasaba na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim ya
watayarishaji bora wa bidhaa za nguo na ngozi bi. Teya ameeleza kuwa ni
mara yao ya 4 kushiriki maonesho hayo na ni mara ya 4 kushinda tuzo
hiyo ambapo awali ilijikita katika bidhaa za ngozi na ila kwa sasa
imejumuisha bidhaa za ngozi na nguo.
Akielezea
changamoto wanazokutana nazo hasa kwenye upatikanaji wa ngozi bi. Taya
amesema kuwa upatikanaji wa bidhaa hiyo hauko vizuri kutokana na uwepo
wa alama zilizowekwa na wafugaji na zile zinazotokana na kuchinjwa hali
inayopelekea ugumu wakati wa kuandaa bidhaa hizo.
Na
ameungana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke akiwaomba watanzania kuunga mkono
juhudi za serikali katika kuelekea uchumi wa viwanda kwa kupenda vya
nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akimuelezea mwananchi aliyefika kwenye banda la Woiso Original Products Company Ltd wanaojihusisha na uuzaji wa bidhaa za nguo na ngozi wakiwa washindi kwenye kipengele hicho kwa mara ya nne mfululizo katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Meneja Masoko wa Kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman akieleza jambo kwa mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akieleza jambo kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman alipotembelea banda hilo na kujionea bidhaa zinazotengenezwa na watanzania zikiwa zenye ubora katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Meneja Masoko wa kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman akizungunza na Globu ya Jamii akielezea tuzo ya ushindi waliyoipata katika kipengele cha Bidhaa za nguo na ngozi kutoka Tanzania ikiwa ni mara ya nne mfululizo wakishinda katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza na Globu ya Jamii akiwa ndani ya banda la washindi wa bidhaa za nguo na ngozi akielezea umuhimu wa watanzania kupenda vitu vya nyumbani ikiwemo kuwaunga mkono Wazalishaji wa ndani wa Viwanda vidogo na vikubwa.
No comments