Ufaransa watwaa ubingwa wa dunia

Jumapili ya July 15 2018 ilichezwa game ya fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ufaransa dhidi ya timu ya taifa ya Croatia katika uwanja Luzhniki nchini Urusi wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 81000. Ufaransa ambao wamewahi kutwaa taji hilo mara moja kabla ya leo na kufika fainali mara kadhaa walicheza dhidi ya Croatia, ambayo ndio mara yake ya kwanza kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo, Croatia imepoteza mchezo na kuishia kupata magoli mawili yaliofungwa na Ivan Perisic dakika ya 28 na Mario Mandzukic dakika ya 69. Rekodi na historia imefanikiwa kuwabeba Ufaransa baada ya kufanikiwa kuifunga Croatia kwa magoli 4-2, magoli ya Ufaransa yalipatikana kwa Mario Mandzukic kujifunga dakika ya 19, Antoine Griezmann kwa mkwaju wa penati dakika ya 38, Paul Pogba dakika ya 59 na Kylian Mbappe dakika ya 65. Kylian Mbappe anaweka rekodi ya kuwa kijana wa pili tokea Pele mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika fainali hiyo. Mlinda mlango wa Ubelgiji Thibaut ametwaa tuzo ya mlinda lango bora zaidi katika fainali hizi. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa taifa hilo kutoa mchezaji bora katika kombe la dunia.

 
 Takwimu za Bingwa
Mechi: 7
Wins: 6
Sare: 1
Magoli ya kufunga: 14
Magoli ya kufungwa: 5


Didier Deschamps anakuwa mwanadamu wa 3 duniani kuwahi kubeba kombe la dunia kama mchezaji na pia akiwa kaama kocha. Wengine ni Mario Zagallo na Franz Beckenbauer.

No comments

Powered by Blogger.