Maagizo aliyotoa Rais Magufuli kwa Kamishna mpya wa Magereza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo July 14, 2018 amemuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Martin Kasike. Tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maagizo Matano aliyoyatoa Rais Magufuli kwa Kamishna Kasike ili aende kutekeleza.
Agizo la Kwanza Rais amemtaka akahakikishie Wafungwa wanafuata taratibu za Magereza “Nataka ukasimamie taratibu za kazi Magereza na uchukue hatua. Sitaki mfungwa atumie simu gerezani” -Rais Magufuli
Agizo la Pili amemtaka Kamishna akahakikishe Wafungwa hawavuti Bangi wala kuongea na simu “Wapo
wafungwa wengine wanazungumza na simu hadi nje ya nchi na Viongozi
wapo, sitaki kwenye Magereza wafungwa wapate nguvu ya kuvuta Bangi na
kujamiana kwa sababu hawapati kazi za kutosha” Rais Magufuli
Agizo la Tatu “Kamishna
nenda ukazikabili changamoto za Magereza, hakuna haja ya kuwa na tatizo
la makazi. Watumieni wafungwa kujenga makazi na wafungwa mlionao
wakipungua wasafirisheni wengine” Rais Magufuli
Agizo la Nne nanukuu “Unakuta
mtu amefungwa, ameacha Mke wake huko nyumbani lakini anakuja mke wake
kwenye gereza anakaribishwa na Askari wa Magereza akafanye mambo ambayo
hakutakiwa kufanya akiwa gerezani” Rais Magufuli
Katika maagizo Rais ametoa pongezi ila zenye maagizo ndani yake “Kamishna
nakupongeza lakini pongezi ni ndogo pole ndio kubwa, najua kuna askari
watakuchukia kwa hatua utakazozichukua na usipozichukua wewe ndiye
utakayenichukia” Rais Magufuli
No comments