Maagizo aliyotoa JPM Magufuli akipokea Gawio la BILIONI 1.5
Rais Magufuli amepokea gawio la Serikali
kutoka Shirika la Simu Tanzania{TTCL} la Bilioni 1. 5 na kuzindua
upanuzi wa huduma za TTCL, katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais magufuli amesema haya yafuatayo wakati akipokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania{TTCL} la Bilioni 1. 5;-
“Kupitia mfumo huu wa ‘TTCL video Conference’ nitawasiliana na wakuu wangu wa mikoa kote nchini na Dr. Shein naye ataitumia kuwasiliana na wakuu wake wa mikoa huko Zanzibar ili kupunguza safari za kila mara mikoani”-Rais Magufuli
“Penye amani kuna biashara, pesa, chakula, ulinzi, uchumi hata dini zitatoa mahubiri mazuri ndipo unapoweza kukemea hata mapepo yakakimbia, pakikosa amani hakuna kukemea. Amani ndio kila kitu” – Rais Magufuli
“Naungana na Watanzania wote kuvipongeza vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, usiku na mchana hawalali kwasababu ya kulinda amani ya watanzania zaidi Milioni 55, endeleni hivyo msikate tamaa. Umma wa Tanzania upo pamoja na nyinyi – Rais Magufuli
“Niwashukuru kwa kuwapatia ajira vijana wa Suma JKT wengine waige hakuna sababu ya kuajiri walinzi toka nje ya TZ, nina uhakika pale Wizara ya kazi kuna matatizo matatizo, nasema kwa dhati napafuatilia” Rais Magufuli
“TTCL isiwe na kigugumizi katika kukusanya madeni yote kwa wateja, vinginevyo mtashindwa kushindana katika soko” Rais Magufuli
“Shirika hili lisiwafie mikononi, itawakuwa ni aibu kubwa, haya mafanikio mliyoyapata katika kipindi kifupi ni sehemu tu ya safari ndefu iliyo mbele yenu” Rais Magufuli
“Sekta ya simu inakuwa kwa kasi sana duniani, watu Milioni 40 Tanzania wanatumia simu za mkononi, huku watu Bilioni 5 duniani wakitumia simu” Rais Magufuli
“Mimi nikisikia siku moja mmezalisha zaidi japokuwa nilishasema hakuna kupandisha mishahara lakini kwa nyinyi mnaozalisha zaidi hata mkipandishwa mishahara ni safi tu” Rais Magufuli
“Gawio hili la Bilioni 1.5 likasaidie kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika kusaidia kwenye bajeti ya mwaka huu 2018/19 nchini” Rais Magufuli
“Vijana wakipewa majukumu wanaweza lakini akitaka kuharibu anaharibu kwelikweli, hii ndo sababu ya kuteua vijana ktk nafasi Serikalini, kwa bahati nzuri wengi niliowateua hawajaniangusha ukiondoa wachache, naahidi kuendelea kuwateua ktk nafasi mbalimbali” JPM

No comments