''Watu wanakamatwa, wanapigwa na kuteswa''>>> Mwita waitara

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh.Mwita Waitara kupitia Chama Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Leo May 25 2018 wakati alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2017/18 alipopewa dakika 5 za kuchangia amesema haya yafuatayo.

Waitara amesema kuwa..."watanzania wote wangetamani watu watoke gizani...Kwanza kuna usumbufu mkubwa sana mtaani ,watu wa Dar Es Salaam na maeneo mengine wanazuiliwa wasitumie mkaa wanakamatwa,wanapigwa na kuteswa na watu wa maliasili lakini gesi ni ghali sana kuliko unavyopatikana umeme..mkitaka ku "save" lazima umeme upatikane kwa bei ya chini na gesi kwa bei nafuu ili wananchi wa "opti" kwamba kununua gunia shilingi Elfu sabini ni nafuu kuliko kulipia umeme"-Mbunge Waitara

"Tanesco mliwapa zao hii wanatakiwa watengeneze utaratibu mwengine wananchi wanalipia umeme zaidi miezi sita unaambiwa nguzo hazipo mita hazipo,hili ni shirika la kibiashara mwenyekiti"amesema hayo Mbunge Waitara

 

No comments

Powered by Blogger.