"Waziri anavaa miwani ya mbao,Tunataka majibu">>>Mbunge Minja
Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja amehoji sababu za Serikali kuvichukulia hatua ikiwemo kivifungia baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti yale yanayotoa taarifa za kuikosoa Serikali lakini haichukui hatua kwa yale yanayotoa lugha chafu kwa vyama vya upinzani.
“Hivi sasa kinachoendela Waziri anafanya kazi ya kufungia magazeti kazi ambayo sio yake, Inasikitisha yale magazeti yanayoandika habari za kuutukana upinzani waziri anavaa miwani ya mbao anakuwa hayaoni lakini yale yanayoikosoa Serikali anavaa miwani ya kawaida na kuyafungia magazeti”–Devotha Minja
No comments