Rais Magufuli aagiza kushughulikiwa waliokula BILIONI 2


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote waliohusika katika ulaji wa fedha BILIONI 2 za mradi wa maji wa Ntomoko.

“Mradi wa Maji wa Ntomoko ambao umeanza Miaka ya 80 mpaka leo 2018 mradi haujakamilika, miradi inayokuja mwaka huu imekamilika lakini huu wa Ntomoko unatomokea tu huko, inawezekana wahusika wapo, walikula BILIONI 2,” amesema Rais Magufuli 

Rais Magufuli akatoa maagizo “Vyombo vya dola na Wizara ya Maji iwatafute waliokula BILIONI 2 washughulikiwe, hatuwezi kubembelezana, Waziri wa Maji, PCCB, Polisi, muwatafute hawa, warudishe pesa zetu au wamalizie mradi wa maji”
 

No comments

Powered by Blogger.