RC Makonda kutoa bima za afya kwa watoto waliotelekezwa Dar (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema kinamama wote waliofika ofisini kwake wakiwa na watoto kwaajili ya kupatiwa msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa atawapatia kadi za Bima ya Afya (Toto Afya Card) bure kwaajili ya matibabu ya watoto wao. 
  
RC Makonda amesema kadi hizo zitatolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 17 kwa kila mama aliefika ofisini kwake pasipokujali idadi ya watoto alionao.

Uamuzi huo umekuja baada ya RC Makonda kujionea mateso wanayopata kinamama hao ikiwemo watoto kuugua Magonjwa yanayohitaji garama kubwa za matibabu na kwakuwa wengi wa kinamama hao wana hali ngumu kimaisha wanashindwa kumudu garama na kusababisha maumivu na mateso kwa mtoto.

 

No comments

Powered by Blogger.