Mama wa mtoto aliyedai baba yake ni Lowassa afunguka (Video)
Baada ya siku ya jana binti mmoja kujitokeza kwa RC Makonda akidai yeye
ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kuomba
kuonganisha na familia ya mzee huyo, Jumatano hii Mama wa binti huyo
amejitokeza kwa RC Makonda na kuzungumzia kwanini mtoto wake huyo
amejitokeza sasa na kueleza kwamba baba yake ni mzee Lowassa. Mapema
jana mtoto mkubwa wa Edward Lowassa aitwaye, Fred alisema hao kama
familia hawatambui kama wanandugu kama huyo.
No comments