RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI (+VIDEO)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
 

Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa
serikali. 

 

No comments

Powered by Blogger.