DSTV watimiza ndoto ya harusi ya vijana wa Kitanzania (+Video)
Wasanii wa muziki Bongo wanofanya vizuri kwa sasa, Nandy na Aslay usiku
wa leo wameweza kukonga nyoyo za mashabiki wao pamoja na maharusi wa
usiku huo Solomon na Magreth, baada ya wawili hao kutumbuiza.
Kupitia king’amuzi cha DSTV katika chaneli yao ya Maisha Magic Bongo wamefanikisha harusi ya ndoto ya vijana wawili wapendanao Solomon na Magreth usiku wa tarehe 28 Mwezi wa nne katika ukumbi wa King Solomon uliopo maeneo ya Osterbay.
Solomon na Magreth wameweza kughaamiwa harusi yao ikiwemo hadi mavazi waliovaa usiku huo, hii ni baada ya wawili hao kuingia katika mchakato ulioandaliwa na DSTV wa kugharamia harusi ya watu wawili waliopanga kufunga ndoa mwaka huu 2018.
Msanii wa muziki Nandy amefunguka na kueleza kuhusu kuingia katika maisha ya ndoa huku akisema kuwa ndoa ni ndoto ya kila mwanamke na kila kitu kinaenda na muda
Mkali wa kutoa ngoma za Bongo Flava mfululizo, Asaly ameeleza ukaribu wake na Nandy ni wakazi tu na sio kama wao ni kundi la muziki ila mashabiki wanavutiwa na ngoma walizofanya pamoja ambazo ni ‘Mahabuba ‘ na ‘Subalkheri Mpenzi’ ndio maana na wanaalikwa katika show pamoja.

No comments