Makamu wa rais azindua siku ya mwanamke wa mfano Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika harakati za Uhuru wa nchi hii.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Siku ya Mwanamke wa Mfano Tanzania iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Makamu wa Rais alisema Ni dhahiri kuwa wanawake walikuwa na mchango mkubwa sana.
Walifanya kazi kubwa katika uhamasishaji, malezi ya watoto na vijana na kusimama bega kwa bega na kuunga mkono wanaume waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano. Walifanya mengi nyuma ya pazia ambayo yalikuwa na mchango mkubwa katika Taifa letu.
Mapenzi yao, subira yao na mchango wao wa hali na mali ndio uliowapa nafasi wanaume kufanikisha harakati za uhuru kwa kuwa wanawake waliwapa wepesi kwa kuwapunguzia mzigo mzito uliokuwa mabegani mwao. Haiyumkini, katika ngao yetu ya Taifa, ikatambua nafasi ya mwanamke kwa kuwekwa sambamba na mwanaume.
No comments