‘Kiongozi shupavu’ Abbas Kandoro aliliwa na Rais Magufuli
Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa RC wa zamani, Abbas Kandoro kilichotokea jana April 27, jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
“Nimepokea
kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro,
nawapa pole wana familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na
msiba huu, pamoja na wananchi wa mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam,
Mwanza na Mbeya ambako aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa.” -Rais Magufuli
“Tumempoteza
mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi kwa umma katika nyadhifa
mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa
halmashauri hautasahaulika.” -Rais Magufuli
“Abbas
Kandoro alikuwa kiongozi shupavu, aliyejiamini na kutekeleza majukumu
yake kwa kuzingatia sheria na taratibu, aliwapenda watu aliowaongoza na
alidhirisha uzalendo wa kweli.” -Rais Magufuli
“Nimesikitishwa
sana na kifo chake, nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira,
uvumilivu na ustahilivu katika kipindi hiki cha majonzi na pia namuombea
Marehemu Abbas Kandoro apumzike mahali pema peponi, Amina” -Rais
Magufuli
No comments