Vanessa Mdee katika stori zinazo Trend Paris Ufaransa

Staa wa muziki wa bongo Fleva Vanessa Mdee awaacha mashabiki zake midomo wazi baada ya kuzungumza lugha ya kifaransa akiwa katika mahojiano na France 24   Paris hii ni kutokana na wengi kuzoea kumuona akizungumza lugha ya Kiswahili pamoja na Kiingereza.

Vanessa Mdee amelelewa na kukulia nchi tofauti ikiwemo Marekani, France,Tanzania na ndio sababu kubwa ambayo imemfanya yeye kujua kuzungumza lugha ya Kifaransa kutokana na kukulia Paris
Vanessa Mdee katika stori zinazo Trend kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufanya mahojiano hayo na pia kuhusu kutangaza tour yake “The Tanzania Money Mondays Tours” ambayo hajasema itaanza lini rasmi na ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram.

Salaam kutoka “City of Lights”, mji niliyokulia, PARIS 🇫🇷. Leo, ninayo furaha ya kuwatangazia nitaungana na @officielfredericgassita kwenye “Live in Concert” tarehe 9 Juni, Libreville, Gabon. Aidha, @mdeemusicofficial inatambulisha rasmi ‘ The Tanzania Money Mondays Tour”, tarehe za karibuni” - Vanessa Mdee

No comments

Powered by Blogger.