Ronaldo hazuiliki, ajitengenezea rekodi mpya kwenye soka

Mshambuliaji hatari wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidi kujitengenezea rekodi katika timu hiyo.


Usiku wa jana mchezaji huyo amefanikiwa kufunga hat-trick yake ya 50. Katika mchezo huo ambao Madrid walicheza na Girona, Ronaldo alifanikia kufunga magoli manne katika ushindi wa mabao 6-3 ambao Madrid wameupata.

Ronaldo alifunga magoli hayo dakika ya 11, 47, 64 na 90 wakati magoli mengine yalifungwa na Lucas Vazquez dakika ya 59 na Bale kwenye dakika ya 86.

Wakati huo hu magoli ya Girona yalifungwa na Cristian Stuani, aliyefunga mabao mawili (29 na 67) na Juanpe (88).

Kwa sasa Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa kufunga mabao kwenye La Liga msimu huu akiwa na mabao 22, wakati Lionel Messi akiongoza akiwa tayari ameshafunga mabao 25.

No comments

Powered by Blogger.