Black Panther yazidi kutikisa dunia, yaingiza dola bilioni 1.182
Filamu ya ‘Black Panther’ imezidi kufanya vizuri katika mauzo yake duniani.
Filamu hiyo imetajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 605.4 kwa Marekani ndani ya mwezi mmoja tangu ilipotoka February 16 ya mwaka huu, pia imeingiza kiasi cha dola bilioni 1.182.5 duniani kote.
filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Marvel Studios, imevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye box office.
Black Panther ambayo imeongozwa na Ryan Coogler, ilitumia bajeti ya kiasi cha dola milioni 200–210 katika kuitengeneza.
Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.
No comments