Naibu Waziri wa Madini baada ya kukuta Mgodi umefungwa,atoa Agizo

agizo alilolitoa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa mgodi wa Nyakavanglaa ndani ya wiki mbili uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.

 Biteko ameyasema hayo kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne,wakati wa kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa mgodi huo.

 “Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao,-Biteko

 “Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati -Biteko

No comments

Powered by Blogger.