Madini ya Tanzania kutoenda kupimwa nje ya nchi
Tanzania imeingia katika ramani ya kimataifa ya upimaji wa madini baada ya kampuni ya madini ya Nesch Mintech kutokea Tanzania kutambulika kimataifa katika upimaji wa madini. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa NESCH, Happiness Nesvinga amesema kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuyapima madini yake bila kuyapeleka nje ya nchi.
“Kwa sasa Tanzania itatambulika rasmi kimataifa katika upimaji wa madini kupitia kampuni yetu, ambapo cheti cha utambulikaji huo kimetolewa na Jumuiya ya Kimataifa inayohusika na madini ISO.” – Nesvinga
Nesvinga amesema awali madini ya Tanzania yalikuwa hayajulikani kimataifa kwa sababu mengi yalikuwa yanapelekwa kupimwa nje ya nchi na hii itasaidia kukuza uchumi wa Tanzania ambapo wawekezaji wa madini watakuwa na uaminifu dhidi ya madini yanayotoka nchini.
No comments