Magari yalivyoteketea kwa moto Liverpool

Magari hayo yalikuwa yameegeshwa kwenye ghorofa la kuegesha magari la King’s Dock karibu na ukumbi wa Liverpool Echo Arena, ambapo inaelezwa kuwa ni miongoni mwa mioto mibaya zaidi iliyowahi kutokea katika maeneo hayo. Katika taarifa iliyotolewa na Polisi jijini humo, imebainisha kuwa iliwalazimu kuwahamisha wakazi wa maeneo hayo na kuwapeleka kwenye makazi ya kudumu ili wasikumbwe na madhara ya moto huo ambao ulikuwa ukianza kusambaa kwenda kwenye majengo mengine.

No comments

Powered by Blogger.