Waziri Jafo apongeza Ujenzi ofisi za halmashauri – KIBITI

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Kibiti kwa Ujenzi mzuri wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya Kibiti mradi unao tarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu. Waziri Jafo alitoa pongezi hizo Leo hii alipokuwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kibiti Mkoani Pwan



Ujenzi huo unaojengwa na mkandarasi SUMA JKT chini ya Mshauri Chuo Kikuu cha Ardhi umemridhisha sana Waziri Jafo kutokana na kuzingatiwa kwa viwango vya ubora katika ujenzi huo. Hata hivyo Jafo ameagiza kuongezwa kwa kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kabla ya mwezi Julai mwaka huu 2019.
 

Katika kuhitimisha ziara yake wilayani humo waziri Jafo ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kutumia fursa waliyonayo ya tofali nzuri zenye ubora zinazo zalishwa na SUMA JKT katika ujenzi wa hospitali yao ya wilaya ambapo hadi sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.5 za ujenzi wa hospitali hiyo.


Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Seif Ungando ameishukuru sana Serikali ya DKT. John Magufuli kwa msaada mkubwa wa miradi ya maendeleo inayoelekezwa wilayani Kibiti.

No comments

Powered by Blogger.