Real Madrid kizimbani kutetea Ubingwa wa Dunia vs Al Ain FC

Msimu wa tatu mfululizo Real Madrid inafika fainali ya Klabu Bingwa ya dunia, lakini safari hii wanaingia uwanjani bila Cristiano Ronaldo ambaye mwanzoni mwa msimu alijiunga na club ya Juventus, Real Madrid wamefika fainali baada ya kuwafunga Kashima Antlers 3-1 siku ya Jumatano.

Katika mchezo wa fainali Real Madrid watacheza dhidi ya Al Ain FC kutoka Falme za Kiarabu. Fainali za Klabu bingwa ya Dunia mwaka huu zinachezwa katika jiji la Al Ain, Abu Dhabi ambapo ndio nyumbani kwa club ya Al Ain FC. Al Ain FC wao wamefika fainali baada ya kuwafunga River Plate kwa mikwaju ya penati siku ya Jumanne.

Mchezo wa fainali utapigwa leo Jumamosi majira ya saa 1:30 Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee.

No comments

Powered by Blogger.