Mwanamke wa kiafrika kupata Ubunge Pakistan “Najihisi Mandela”

kutoka huko nchini Pakistan ambapo Mwanamke aitwae Tanzeela Qambrani mwenye miaka 39 na asili ya Tanzania ameteuliwa kuwa Mbunge nchini humo na kuwa Mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwa Mbunge nchini Pakistan.
 
Tanzeela ameteuliwa na chama chake cha Pakistan People’s Party (PPP) na kuapishwa Jumatatu ya August 14 akiwa amevalia mavazi ya Kiafrika na amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba alijihisi kama Nelson Mandela wakati akiapishwa.

Inaelezwa kuwa Tanzeela ambae amekuwa mtetezi wa elimu na haki za Wasichana nchini humo ametokea kwenye jamii Sidi ambayo ndio jamii ya Watu wenye asili ya Afrika ambao hubaguliwa sana nchini humo.

Inadaiwa kuwa Mababu wa Tanzeela ambae ni mtaalamu wa masuala ya Kompyuta walitokea Tanzania kabla ya kuingia nchini humo huku Dada yake mmoja na Tanzeela anatajwa kuolewa nchini Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.