Rais Magufuli kuongoza mapokezi ya ndege Hapo kesho

 
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli hapo kesho siku ya Jumapili 8,2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania.

Ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 Mchana, ikitokea Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya 4 kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuliwezesha shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kuimarisha huduma zake.

No comments

Powered by Blogger.