RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM

UKOMBOZI wa sasa kwa vyama tawala katika nchi za Afrika  ni vema wakajikita katika katika kujenga uchumi katika sekta mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.John Magufuli wakati akifungua Mkutano wa Vyama vya siasa ambavyo vilivyopigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambapo vina uhusiano na Chama cha Kikomonisti cha China (CPC) uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Rais Dk.John Pombe Magufuli amesema kuwa chama cha CPC kimekuwa na uhusiano ya muda mrefu na kilisaidia ukombozi katika Afrika kwa kutoa silaha lakini sasa wamekuwa na maendeleo ambapo lazima kujifunza kutoka kwao.

Amesema kuwa nchi za Afrika zitoke katika mnyororo wa unyonyaji na kuingia katika uchumi wa kujitegemea. Amesema kuwa nchi ya China imekuwa ikitoa msaada bila masharti na kwamba kinachofanyika maelewano na msaada unatoka.


   
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

   
 Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.

   

Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

   
Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam

No comments

Powered by Blogger.