Sababu kesi ya Mbowe kukwama kusikilizwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayowakabili Viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe hadi June 27,2018 kwa sababu Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji hakufika mahakamani. 

 Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada wakili wa serikali, Faraja Nchimbi kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali lakini mshtakiwa wa 6, Dk.Vicent Mashinji hayupo mahakamani. 

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa Dk.Mashinji ana udhuru yupo katika mahakama ya Songea ana kesi nyingine, hivyo wanaomba ahirisho. 

 Maombi hayo ya ahirisho yaliibua mvutano wa kisheria baada ya wakili wa serikali Paul Kadushi kutaka kesi iahirishwe hadi kesho, huku wakili Kibatala akitaka iahirishwe hadi tarehe nyingine.

 Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 27,2018 Mbali ya Mbowe na Mashinji, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika. 

Pia mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

 Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, ambapo inadaiwa  February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

No comments

Powered by Blogger.