Real Madrid kubeba kombe la CL mara 3 mfululizo

 Liverpool hii leo pamoja na ubora wao wote walikubali kipigo cha mabao 3 kwa 0 kutoka kwa Real Madrid.

dakika ya 26 baada ya Sergio Ramos kumchezea rafu mbaya Mo Salah ambayo ilimfanya kwenda nje dakika 5 baadae, hata hivyo hadi dakika 45 za kwanza zinaisha ilikuwa Real Madrid 0-Liverpool 0.

 
Dakika ya 51 uzembe wa mlinda lango wa Liverpool Loris Karius ulimfanya Karim Benzema kuwapa Madrid bao la uongozi, bao hili ni la 56 kwa Benzema na anakuwa mchezaji wa pili wa Kifaransa kufunga katika fainali ya CL baada ya Zinedine Zidane 

 
Dakika ya 55 Sadio Mane aliisawazishia Liverpool na hili likiwa bao lake la 10 katika CL msimu huu na la 20 kwa msimu huu, dakika ya 61 Zinedine Zidane alimnyanyua Gareth Bale aliyekuwa benchi na sub ya Gareth Bale ilibadili kila kitu katika mchezo huo.

 
 Real Madrid wanakuwa timu ya kwanza kubeba kombe la CL mara 3 mfululizo baada ya Bayern Munich 1974-1976, na timu za Uingereza sasa zinakuwa zimepoteza katika fainali 7 za mwisho za Ulaya dhidi ya timu kutoka Hispania.
 

No comments

Powered by Blogger.