Mwigulu; “Lengo sio kuminya uhuru wa maandamano kwani yapo kikatiba”
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba ameonya kuhusu maandamano yanayopangwa kwani ndani yake watakuwepo watu ambao watafanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.
Waziri Mwigulu ameeleza kuwa lengo la serikali si kuminya uhuru wa maandamano kwani yapo kikatiba bali wapo watu ambao watatumia mwaya wa maandamano hayo kuvuruga amani ya nchi.
“Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesivyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza.” – Waziri Mwigulu
No comments