Chanzo cha Moto kuzuka katika Mahakama ya Kisutu

March 1, 2018 Kumetokea hali ya taharuki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar Es Salaam baada ya kutokea kwa mlipuko wa moto uliosababishwa na Transfomer
 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Mahakama hiyo, Gasto Kanyairita amesema kuwa moto huo umetokea majira ya saa 4 asubuhi,wakati mlipuko huo unatokea kulikuwa na kesi nyingi zikiendelea mahakamani. 

 “Baada ya kufatilia tulibaini kuwa ni transformer ambapo ilisababisha kuungua kwa waya wa TTCL, simu na Internet ambapo shughuli za mahakama zilisitishwa kwa muda,” -Gasto Kanyairita 

 “Niwatoe hofu Watanzania mlipuko uliotokea ni wa shoti ya umeme na ni kawaida kutokea, hivyo waepukane na taarifa za uongo,”-Gasto Kanyairita 

 “Ilitubidi tutoke nje kutokana na hofu tuliyokuwa nayo, lakini tunashukuru hakuna madhara yoyote ya kibinadamu,”-Shuhuda

No comments

Powered by Blogger.