Al Masry vs Simba wamaliza kazi Port Said Misri


Wekundu wa Msimbazi Simba safari yao ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Africa CAF, imehitimishwa leo katika uwanja wa Port Said nchni Misry baada ya kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Masry.

Simba SC katika mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiwa nyumbani ilifanya kosa  la kuruhusu kufungwa magoli mawili katika mchezo uliyomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, hivyo leo walikuwa wanahitajika kupata walau ushindi wa kuanzia goli 1-0 au sare ya kuanzia 3-3.

Kwa bahati mbaya Simba wameshindwa kupata matokeo ugenini dhidi ya Al Masry na kujikuta wakilazimishwa sare tasa (0-0), hivyo kutokana na mchezo wa kwanza wa nyumbani walitoka sare ya 2-2, wanaondolewa katika michuano hiyo kwa goli la ugenini, hivyo sasa amesalia katika michuano ya Ligi Kuu pekee.

No comments

Powered by Blogger.