Sugu ameachiwa kwa dhamana,RCO Mbeya amtetea
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga wanaokabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wote wawili baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia Mahakama ameshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.
Hakimu Mteite amekubaliana na hoja hiyo ya Mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa February 26, 2018 “Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya shilingi Milioni 5 kila mmoja"
.

No comments