“Mwigulu, Masauni na IGP Sirro wanasubiri nini ofisni”>>> CHADEMA ,+VIDEO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani Dr. Mwigulu Nchemba, Naibu wake Engineer Masauni pamoja na IGP Simon Sirro wajiuzulu kufuatia kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina

 Akiongea na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema muendelezo wa matukio haya ikiwemo la mwanafunzi ni utamaduni mpya katika siasa ambao ni muendelezo wa kushambuliwa kwa watu mbalimbali akiwemo Tundu Lissu

 “Tunalaani na tunasikitishwa na mauaji yaliyofanywa kwa mwanafunzi huyu, kwani huu ni muendelezo wa matukio ya mauaji na kuteka watu,”-Mrema 

“Tunamtaka Masauni na Mwigulu wakumbuke Mwinyi alijiuzulu wakati wafungwa walipofia Gerezani Shinyanga, IGP anafanya nini Ofisini, Mwigulu anafanya nini ofisini, hivyo tunataka waachie Ofisi,” -Mrema. 

 

No comments

Powered by Blogger.