Mwanamume amekamatwa na Dawa za Kulevya kwenye makalio
stori kuhusu ishu ya dawa za kulevya ambapo Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia.
Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil. Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundua hilo. Mwanamume mwingine ambaye anatuhumiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo.
Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamesafirishwa kutoka Amerika ya Kusini.
No comments