Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena kizimbani
Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao.
Namnukuu Hamisa Mobetto akizungumza nje ya Mahakama “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto, Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na tumeridhika, hivyo yamekwisha”
“Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani. Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto” Diamond Platnumz
No comments