Professa Ndalichako azitaka halmashauri zote kujenga mabweni ya shule za sekondari ili........soma zaidi

waziri wa elimu sayansi na teknolojia Joyce Ndalichako azitaka halmashauri zote nchini kujenga mabweni ya shule za sekondari kuepusha changamoto zinazokwamisha masomo ya wanafunzi. Amesema hayo mkoani Njombe hapo jana wakati aliposhiriki harambee kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya Sovi inayoelezwa kuwa na wanafunzi NANE waliobainika kuacha masomo kutokana na kupata Ujauzito. pia Mheshimiwa Ndalichako anasema "bado kunakuwa na wanafunzi wanaolazimika kutembea umbali mrefu kufika shuleni na hii inawapunguzia utulivu wa kujifunza,kwa hiyo anaomba kuiga mfano kujenga mabweni".

No comments

Powered by Blogger.