Prof. Benno Ndulu kutunukiwa Tuzo ya Gavana Bora Barani Afrika
Gavana Mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu, May 22, ametunukiwa tuzo ya Gavana Bora Barani Afrika kwa mwaka 2018 inayotolewa na jarida maarufu la African Banker Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimefanyika jijini Busan, Korea Kusini.
“Hii tuzo nimepewa mimi kutokana na mchango mkubwa kutoka BoT wakati wa uongozi wangu. Kwa hiyo, tuzo hii ni heshima kubwa kwangu na kwa Benki Kuu ya Tanzania,” alisema katika mahojiano jijini DSM.
“Awali niliwaomba waandaaji nao walikubali kwamba Dkt. Namajeje Weggoro, Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki apokee tuzo hiyo kwa niaba yangu. Sikujua kama Naibu Gavana wa BoT, Julian Banzi Raphael, anashiriki katika mikutano ya AfDB, vinginevyo yeye ndiye angepokea kwa niaba yangu,” -Prof. Ndulu
Prof. Ndulu ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza huduma jumuishi za kifedha na kuchangia katika kuhakikisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanafikiwa na huduma rasmi za kibenki.
No comments