Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge
Mapema
leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha
Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili
Thelathini na Mbili Elfu.
Kati
ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia
Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa
ajili ya bajeti ya maendeleo.
Pro.
Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba
ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu
Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba. Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma .
Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma
No comments