IGP na AG waitwa Mahakamani kujibu kuhusu Abdul Nondo


  kuhusu Mwanafunzi Abdull Nondo, ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa wito kwa Mkurugenzi wa Upelelezi Tanzania (DCI), Mkuu wa Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani hapo kujibu hoja kuhusu Nondo kutofikishwa mahakamani.
 
Wakili wa kujitegemea, Jebrah Kambole amesema wamewasilisha maombi kuhusu Nondo katika Mahakama hiyo tangu Ijumaa iliyopita wakiwa na hoja tatu,Amesema maombi hayo wanaomba apewe dhamana, ama apelekwe mahakamani ama aachiwe huru.

 “Tangu aletewe Dar es Salaam hakuna aliyeonana naye si ndugu, mawakili wala wanafunzi wenzake na hajafikishwa mahakamani hivyo tumeona njia ya pekee ni kwenda mahakamani kwa sababu ana haki ya kupata dhamana kama watu wengine,” -Jebrah.

“Mahakama imetoa wito kwa viongozi hao ambapo wametakiwa kufika mahakamani March 21, 2018 -Jebrah 
 
 

Mwigulu ametamani kumuona Nondo chuoni, aongelea yeye kujiuzulu

No comments

Powered by Blogger.