“Serikali itagharamia mazishi ya Mwanafunzi aliyeuawa” -Prof. Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako amesema Serikali itagharamia shughuli za mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Akwilina Maftah aliyeuawa kwa risasi Februari 16, 2018

“Mafunzo yale kwa vitendo yalikuwa yanatarajiwa kuanza February 26, 2018 hivyo Kifo chake kimeleta simanzi kwa wananchi wote na Serikali kwa ujumla,”- Prof. Ndalichako

 Ndalichako amesema kuwa Akwilina alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa kike waliojipambanua kwa kujua umuhimu wa elimu , alihakikisha kwamba anasoma kwa bidii kwa manufaa yake na familia yake, lakini pia alikuwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu 

 

No comments

Powered by Blogger.