Rais Magufuli ameteua Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi umeanza jana February 1, 2018.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA). Pia President JPM amemteua Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG) kuanzia February 1, 2018. Kabla ya Uteuzi huu Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority – TIRA). Kufuatia uteuzi huu President Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Mcheche Masaju na aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kuanzia February 1, 2018. Wote walioteuliwa wataapishwa Jumamosi February 3, 2018 saa 9:00 Alasiri Ikulu dsm

No comments

Powered by Blogger.