Dakika 7 za matokeo ya game ya Real Madrid vs PSG
Game ya Real Madrid dhidi ya PSG ndio ilikuwa game inayotajwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na PSG wamerudi Hispania ikiwa msimu uliyopita PSG wakiwa Hispania aliruhusu kufungwa magoli 6-1 dhidi ya FC Barcelona.
PSG waliingia Hispania katika uwanja wa Santiago Bernabeu wakiwamejizatiti licha ya kuwa wamepoteza tena mchezo kwa magoli 3-1, PSG ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 33 kupitia kwa Rabiot lakini Cristiano Ronaldo aliswazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 45.
Hali ya umiliki wa mchezo ilikuwa ni asilimia 50 kwa 50 kitu ambacho iliwachukua dakika saba kabla ya game kuisha Real Madrid kupata magoli mawili ya ushindi, yaliofungwa na Ronaldo dakika ya 83 na Marcelo dakika ya 86 na kuifanya game imalizike kwa magoli 3-1.
Matokeo ya game za Champions League zilizochezwa February 14
No comments