CHADEMA kuhusu kuyakataa matokeo ya Uchaguzi wa marudio - Tamko

Kumefanyika uchaguzi wa marudio katika Majimbo Mawili Jimbo la Siha na Kinondoni ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa yake kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa marudio uliofanyika February 17, 2018 katika Jimbo la Siha na Kinondoni.

 Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Vicent Mashinji ameeleza kuwa baada ya upigaji wa kura katika uchaguzi kumalizika uligubikwa na vitendo vya viovu vya kihalifu. 

 CHADEMA imeeleza kuwa katika Jimbo la Kinondoni Tume imefanya urasimu kinyume cha sheria na kumefanyika makosa ya makusudi kuhakikisha chama hicho hakiweki Mawakala kwenye vituo vya kupiga kura kwa zaidi ya saa 2 tangu vituo vilipofunguliwa

 Katika Jimbo la Siha CHADEMA imeeleza kuwa vyombo vya Dola, hususani Jeshi la Polisi limetumika kubadili matokeo kwa kuwalazimisha Mawakala kusaini fomu za Matokeo tofauti na fomu rasmi zilizoko vituo na huku wakitumika kupora Masanduku na kubandika matokeo yasiyojulikana yametoka wapi.

No comments

Powered by Blogger.