Wapangaji waambulia Kinyesi baada ya kupandishiwa pato la nuymba a.k.a Kodi

Kenya kwa Rais Uhuru Kenyatta ambapo Wapangaji wa nyumba katika mtaa wa Lang’ata jijini Nairobi, ambao wamekataa kulipa kodi iliyoongezwa na mwenye nyumba wao wamepata mshtuko mkubwa baada ya mwenye nyumba kumwaga kinyesi ndani ya nyumba zao. Wapangaji 40 wa nyumba zinazoitwa Ocean Park Apartments walienda mahakamani kutafuta msaada ili kuzuia mwenye nyumba yao kupandisha kodi na mahakama ikaamua waendelee kulipa Tsh. 540000 kila mwezi ambayo walikuwa wakilipa awali. Mahakama ilimwambia mwenye nyumba, nanukuu “Unashauriwa kurejesha huduma zote kwa mfano maji, umeme, ukusanyaji taka, ulinzi, na huduma za uegeshaji magari mara moja,” Mwenye nyumba hizo anayefahamika kwa jina Joseph Kagwatha alikuwa amewafahamisha wapangaji wake kuhusu kodi mpya na ilitarajiwa walipe Tsh. 650000 kutoka Tsh. 540000 kila mwezi, lakini wapangaji waligoma.

No comments

Powered by Blogger.