Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli apokea masikitiko makubwa kuuwawa kwa Askari 14 JWTZ Congo DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo katika operesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pamoja na askari hao kuuawa, askari wengine 44 wamejeruhiwa na 2 hawajulikani walipo. Kufuatia vifo hivyo Mhe. Dkt. Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mkuuwa Majeshi ya Ulinzi Jenerali. Venance Salvatory Mabeyo, Maafisa na Askari wa wote JWTZ, familia za marehemu na Watanzania wote kwa kuwapoteza mashujaa waliokuwa wakitekeleza wajibu wao.

No comments

Powered by Blogger.