RAIS JPM AKIWASAMEHE BABU SEYA NA PAPII KOCHA

Rais Magufuli ametangaza kuwasamehe familia ya mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanaye Papii Kocha ambao walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha gerezani. Akihutubia taifa katika sherehe za Uhuru mjini Dodoma, Rais Magufuli pia ametangaza kusamehe wafungwa 8,157, na kuagiza wafungwa 1,828 kati yao watolewe magerezani mara moja na waliobaki wapunguziwe muda wa kukaa gerezani ili waje watolewe kwa mujibu wa vifungo vyao.

No comments

Powered by Blogger.